MWANAMUZIKI MBALAMWEZI WA KUNDI LA THE MAFIK AFARIKI DUNIA


Mwanamuziki Mbalamwezi ambaye ni mmoja wa Wasanii  wanaounda kundi la The Mafik amefariki dunia kutokana na majeraha ambayo yanahusishwa na kupigwa.Baadhi ya ndugu wamesema taarifa za awali ni kwamba Mwili wake ulikutwa maeneo ya Africana Dar es salaam ukiwa hauna nguo ikiwa ni saa kadhaa zimepita toka msanii huyo atokomee bila kujulikana alipo. 

Msanii huyo ameshiriki katika kazi za kundi ambazo zimefanya vizuri kama Passenger, Sheba,Carola, Vuruga, na Dodo, pia ameshirikishwa katika nyimbo za Ruby na Ben Pol.

Post a Comment

0 Comments